Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amesema Chadema ni chama cha matapeli na ndiyo maana alihama upinzani.
Mtatiro ambaye chama chake cha zamani cha CUF kilikuwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya NLD, Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 13, 2018 katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Ukonga.
Katika mkutano huo, Mtatiro amesema ameshtuka na mchezo mchafu ulioko Chadema na kwamba wapo kimaslahi.
"Tupo hapa kumsapoti Mwita Waitara, ukiona kiongozi kama mimi niliyekaa miaka kumi na nimeachana na utapeli wewe kijana shtuka kapige kura kwa Waitara," amesema.