Kaka wa Michael Jackson, amchumbia binti wa miaka 23

Kaka wa Michael Jackson, amchumbia binti wa miaka 23
Kaka wa Marehemu Michael Jackson anayejulikana kwa jina la Jermaine Jackson mwenye umri wa miaka 63 ametangaza nia ya kufunga ndoa na binti mwenye umri wa miaka 23 Maday Velazquez.

Wawili hao walikutana kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya kundi la “The Jackson 5” mjini Malloca nchini Hispania mwanzoni mwa mwaka huu 2018, Jermain Jackson ametangaza nia hiyo kupitia chombo cha habari cha “De Telegraaf” kilichopo Uholanzi na kusema “Tutaoana hivi karibuni”.



Jermaine Jackson aliachana rasmi na mkewe Halima Rashid mwaka 2016 na hii itakuwa ni ndoa yake ya nne huku katika ndoa hizo amebahatika kupata watoto 9.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad