SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kukatisha ukuta wa Uwanja wa Taifa kesho Jumapili kama atakuwa hana tiketi ya kuingilia uwanjani.
Simba na Yanga kesho ndiyo mara ya kwanza watakutana katika msimu huu wa 2018/19 mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam saa 11 jioni.
TFF imefanya hivyo ili kuimarisha ulinzi na kuzuia fujo zote ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wamashabiki watakaojitokeza uwanjani hapo kesho.
Kikosi cha timu ya Simba.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kuwa tiketi zitaendelea kuuzwa lakini mwisho itakuwa ni leo Jumamosi na kesho hakutakuwa na uuzwaji katika eneo la Uwanja, lengo ni kuimarisha ulinzi kwa mashabiki ambao watajitokeza uwanjani hapo kushuhudia mchezo huo.
“Kumekuwa na vikao mbalimbali kuhakikisha mchezo huu unakuwa salama kwa kuhakikisha tunaimarisha ulinzi kama inavyofahamika kuwa ni moja ya michezo inayokusanya watu wengi zaidi.
Kikosi cha timu ya Yanga.
“Na mtu yeyote ambaye atakuwa hana tiketi basi siku ya Jumapili asikatize katika ukuta wa uwanja kwani kutakuwa na ulinzi wa kutosha kuhakikisha watu wanaokuja hawapati bugudha yeyote,” alisema Ndimbo. Mpaka jana tiketi 1300 zilikuwa zimeuzwa.
Kama Hauna Tiketi Marufuku Kuonekana Taifa Kesho- TFF
0
September 29, 2018
Tags