Kamati ya Waamuzi TFF Yatoa Tamko Kuhusu Marefarii Mechi ya Simba na Yanga

Kamati ya Waamuzi TFF Yatoa Tamko Kuhusu Marefarii Mechi ya Simba na Yanga
Wakati ikielezwa kuwa Mwamuzi Mwanamama Florentina Zabron atakuwa pilato wa mchezo utakaowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, amesema watatangaza majina rasmi ya waamuzi wote watakaocheza mchezo huo Alhamis.

Chama amesema waamuzi wote wanapaswa kuwa na BEJI ya FIFA kutokana na msisimko wa mechi hiyo ya aina yake yenye ushawishi mkubwa ndani ya soka la Tanzania.

Mwenyekiti huyo amesema wameamua kufanya hivyo ikiwa zitakuwa zimekuwa zimesalia siku tatu kabla ya mechi hiyo kuelekea mechi hiyo.

Aidha, Chama ameeleza kuwa TFF imeanzisha utaratibu mpya wa kuwatangaza waamuzi wa mechi zote za ligi siku tatu kabla ya mchezo husika tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

Simba na Yanga zitateremka dimbani Septemba 30 2018 kwa ajili ya kupigania alama tatu huku Simba wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya mwisho waliyokutana msimu uliopita.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad