Katibu Mkuu wa Zamani wa UN Kofi Annani Azikwa Accra, Ghana

Katibu Mkuu wa Zamani wa UN Kofi Annani Azikwa Accra, Ghana
Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan inafanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Waombolezaji waliovaa nguo nyeusi na nyekundu wamejaa katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa mjini Accra ambako unaweza kupokea takriban watu 4000.

Watu wengine zaidi wamekaa katika ukumbi mwingine nje ya ukumbi mkuu wakitazama kupitia televisheni shughuli zinavyoendelea.

Wageni waheshimiwa kutoka kote duniania wanahudhuria mazishi ya kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wamataifa akiwemo rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast pamoja na katibu mkuu wa sasa Antonio Gutterrez.

Katika hotuba yake, ameeleza jinsi Annan daima alivyotazamia kurudi nyumbani, na ameishukuru Ghana kwa kumleta duniani mtu wa aina yake.

Alimaliza kwa kusema: "Ataendelea kukumbukwa kupitia wakfu wake na kupitia kwetu sote."

Katibu mkuu wa sasa wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amewaambia waombolezaji, wakiwemo baadhi ya viongozi wa Afrika na viongozi wa zamani kwamba wakati Annan akizungumza:

Nukuu ya ujumbe huo: ''Dunia hutegemea kusikiza na tulifaidika kutokana na busara yake."

Kwa muda wa siku mbili zilizopita mwili wake Annan umekuwa ukiagwa mjini humo na watu mbalimbali, wakiwemo watu maarufu.

Viongozi tofuati duniani wanahudhuria mazishi hayo katika makaburi ya jeshi ya Kambi ya Burma mjini Accra.

Mjane wa aliyekuwa rais wa kwanza afrika kusini Nelson Mandela - Bi Graca Machel na Gro Harlem Brundtland ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu nchini Norway ni miongoni mwa wanaohudhuria mazishi ya Annan

Nukuu ya ujumbe wake: ''Daima alitetea amani , na kuwapatia watu kipa umbelekatika mchango wake duniani. Ninampenda kwa dhati, ni kakangu na kwa kweli nilazima niseme, bado sijakubali kwamba ameondoka."

Kofi Annan alihudumu kama Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad