Kijana wa Kiafrika aliemuokoa mtoto apatiwa rasmi uraia na Ufaransa


Kijana mhamiaji kutoka nchini Mali, Mamoudou Gassama maarufu kama 'Spiderman' amepatiwa uraia rasmi wa Ufaransa baada ya jitihada zake kuonekana akimuokoa mtoto mdogo kutoka kwenye ghorofa refu jijini Paris nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu. 

Gassama alipanda haraka ghorofa nne bila kutumia chombo chochote na kumuokoa mtoto huyo wa miaka minne, ambaye alikuwa akining'nia ghorofani huku kukiwa hakuna usaidizi wowote ule. 

Kupitia tukio hilo Gassama alijipatia umaarufu mkubwa duniani baada ya 'video clip' yake kusambaa mitandaoni akionekana  kumuokoa mtoto, ambapo Rais Emmanuel Macron binafsi alimshukuru kwa ujasiri wake na kuahidi kumpa kazi katika kikosi cha zimamoto. 

Awali, Gassana alipewa hadhi ya ukazi wa Ufaransa, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kupata uraia rasmi wa Ufaransa. 

Mbali na hilo, mnamo Juni 24 Gassama aliweza kutwaa tuzo ya BET kipengele cha "Humanitarian Awards", ambayo alipatiwa kutokana na kitendo chake cha ushujaa kilichoonekana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad