Nchini Ufilipino Watu zaidi ya 25 wamefariki dunia na wengine 13 hawajulikani walipo kutokana na Kimbunga, ambapo wengi wao walikuwa wakiishi maeneo ya Milimani.
Kimbunga hicho kiitwacho Mangkhut, kinachukuliwa kuwa chenye nguvu zaidi hakijawahi kutokea eneo hilo, kikiwa na upepo unaosafiri Kilometa 200 kwa saa.
Leo, Jumapili kimbunga kimeonekana kikipita katika Bahari ya Kusini mwa China kuelekea katika Jiji la Hong Kong na Pwani ya China.
Aidha, mapema leo asubuhi Mamlaka za Hong Kong zimeonesha ishara ya juu ya alama 10 ya dhoruba baada ya upepo mkali kuanza kupiga madirisha ya juu katika majengo marefu huku mawimbi ya bahari yakionekana kuongezeka nguvu.
Mamlaka ya anga pia imezuia safari zake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hong Kong ili kujihami na Kimbunga hicho.