Kiongozi wa Yanga atuma ujumbe huu Simba

Kiongozi wa Yanga atuma ujumbe huu SimbaAliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Yanga na sasa Meneja wa kikosi, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kurejea kwa mshambuliaji wao Amis Tambwe ndani ya dimba kumeasha ari kuelekea mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba.

Cannavaro ameeleza kuwa Tambwe amekuwa mchezaji wa kucheka na nyavu kwa muda mrefu haswa pale anapopata nafasi nzuri ndani ya uwanja hivyo hana wasiwasi naye.

Meneja huyo aliyewahi kucheza Yanga kwa mafanikio makubwa, anaamini kitendo cha Tambwe kufungua akaunti ya mabao juzi dhidi ya Singida United kitamwamsha na kujiweka fiti zaidi.

Aidha, Cannavaro ameeleza kuwa mechi yao dhidi ya Simba ni ya kawaida hivyo maandalizi yao yatakuwa kama mechi zingine za ligi.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Singida United, Tambwe alipachika kambani mabao mawili na kuwamaliza Singida United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad