Kisa Simba Mzee Akilimali Aiwakia Yanga Ataka Uchaguzi Ufanyike Haraka

Kisa Simba Mzee Akilimali Aiwakia Yanga Ataka Uchaguzi Ufanyike Haraka
Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amesisitiza kwa kuutaka uongozi wa Yanga kuhakikisha unafanya uchaguzi mpya haraka ili kumpata Mwenyekiti wa klabu hiyo.

Kauli ya Akilimali imekuja tena kutokana na uongozi wa Simba jana kutangaza kuwa itafanya uchaguzi wake Novemba 3 2018 ili kupata viongozi wapya ambao watachukua nafasi za waliomaliza muda wao.

Mzee huyo ameongea kwa jazba akishangaa kuwa mpaka sasa Yanga haijafanya uchaguzi wakati ndiyo ilikuwa klabu ya kwanza kupaswa kufanya hivyo.

Katibu huyo ameeleza kushangazwa na namna Yanga wanachokitaka huku akisema ni jambo la kushangaza kwa maana hata klabu ya Coastal Union tangu iamuliwe na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanua uchaguzi ilikamilisha haraka.

Aidha, Akilimali amesema mpaka sasa aliyekuwa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji, hajasema kama amerejea na kwa mujibu wake haoni haja ya kumbembeleza mtu ambaye hana nia ya kurejea.

Yanga na Simba zote zilipewa siku 75 za kuanza mchakato wa uchaguzi na TFF na Simba wametangaza jana tarehe rasmi ya uchaguzi huo ambapo fomu zitaanza kutolewa leo kunako makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Msimbazi, Dar es Salaam.
HABARI ZAIDI KAMA HIZI SOMA KUPITIA APP YA UDAKU SPECIAL

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad