Kocha wa Braz Ajibu Vijembe vya Trump

Kocha wa BrazAjibu Vijembe vya Trump
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Tite amejibu vijembe vya Rais wa Marekani, Donald Trump alivyovitoa kwa timu ya taifa ya nchi hiyo kwenye Ikulu yake ya ‘White House’.

Mwezi uliopita, Rais wa shirikisho la soka duniani, Gianni Infantino alitembelea Ikulu ya Marekani, ndipo Rais Trump alipoonekana kuipiga vijembe timu ya jaifa ya Brazil kufuatia kutolewa kwake katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi.

Alipokuwa akijibu swali la mwanahabari mmoja wa Brazil katika ziara hiyo, Rais Trump alimpiga kijembe kwa kusema,

Taifa la soka…. Nafikiri mmepata tatizo hivi karibuni"

Naye kocha wa Brazil alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Rais Trump katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya El Salvador utakaochezwa nchini Marekani hii leo, Tite amesema,

"Jibu langu kwa Rais Trump ni kwamba tumeshinda kombe la dunia mara tano, nafikiri kihistoria atakuwa anatufahamu vizuri zaidi".

Brazil itacheza mchezo wake wa pili wa kirafiki dhidi ya El Salvador baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Marekani kwa mabao 2-0 .

Katika mchezo huo dhidi ya Marekani, mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, Neymar Jr alikabidhiwa unahodha wa kudumu wa timu ya taifa ya Brazil ambapo alifunga bao lake la 58 kwenye timu hiyo linalomuweka nafasi ya tatu katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo.

"Neymar anaweka rekodi muhimu na inayovutia, na ana uzalendo mkubwa kwa nchi yake ambao daima ataendelea kuuonesha. Ataweza kuongoza katika mchezo wa leo kwasababu kuna vitu tunahitaji kuvisimamia, kwanza kabisa timu ya Brazil inatakiwa kucheza vizuri na kushinda", amesema Tite alipomzungumzia nahodha wa timu hiyo, Neymar Jr.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad