Kocha Yanga Aweka Rekodi ya Aina Yake Taifa

Kocha Yanga Aweka Rekodi ya Aina Yake Taifa
Baada ya kukishuhudia kikosi chake mbashara kikicheza dhidi ya Stand United, Kocha wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, juzi aliweka rekodi ya kukaa kwa mara ya kwanza kwenye benchi la ufundi.

Kocha huyo ambaye alikuwa hana kibali cha kazi kwa muda mrefu, alikuwa sehemu ya benchi la ufundi katika Uwanja wa Taifa ikiwa ni mara ya kwanza tangu awasili nchini.

Zahera alianza kukaa kwenye benchi hilo wakati Yanga ikicheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, mechi ambayo walifungwa bao 1-0.

Mkongomani huyo ameweka rekodi hiyo tangu kuondoka kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina aliyeondoka bila kuaga kutokana na kutofikiana mwafaka kwa baadhi ya mambo na mabosi wake wa zamani.

Wakati huo kikosi cha Yanga kitaendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Jumatano ya wiki hii.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad