Kofi Annan Kuzikwa leo Accra, Ghana

Hatimaye Kofi Annan Kuzikwa leo Accra, Ghana
Mwili wa aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan unatarajiwa kuzikwa hii leo katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Kwa muda wa siku mbili zilizopita mwili wake ulikuwa ukiagwa mjini humo na watu mbalimbali, wakiwemo watu maarufu.

Viongozi kadhaa wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo katika makaburi ya jeshi ya Kambi ya Burma mjini Accra.

Kofi Annan alihudumu kama Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006.

Kifo cha Annan: Viongozi nchini Kenya watuma rambi rambi zao
Kofi Annan amtaka Odinga kutumia njia za kisheria Kenya
Waombolezaji waghadhabishwa na hatua ya kuzuiwa kuona mwili wa Annan Ghana
Leo inahitimisha kilele cha wiki kadhaa ya maandalizi ya mazishi yake, ambaye ni mmoja wa wana diplomasia wanaoheshimika duniani.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Accra anasema kuwa, ngoma za maombolezo zilisikika mfululizo kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Accra, sehemu ambayo mwili wake ulikuwa ukiagwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad