Kope, kucha bandia zamuibua Vicky Kamata


Mwanamuziki wa zamani na Mbunge wa viti maalum (CCM), Vicky Kamata amewataka wasanii wa kike nchini kujitafakari kwa kina kuhusu utumiaji wa vitu bandia hasa kucha na kope kwa kudai vitu hivyo vinaweza kuwasababishia maradhi makubwa ambayo yatasababisha  kushindwa kutekeleza majukumu yao. 

Vicky amesema licha ya mwanamke kuumbiwa urembo lakini wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa katika utumiaji wa vitu hivyo ambavyo kwa sasa vimebainika kuwepo na athari kubwa ikiwemo saratani ya ngozi. 

"Binafsi nimepokea kawaida tu kuhusu suala hilo ila nafikiri hii mada ni vizuri wakajengewa imani wakina mama wajiamini jinsi walivyo na kuacha kutumia au kujiwekea vitu vya nyongeza katika miili yao. Sioni haja ya kuendelea kuwepo vipodozi hivyo na kuendelea kutumiwa kama kweli vinaleta madhara", amesema Vicky. 

Pamoja na hayo, Vicky ameendelea kwa kusema "wasanii wajipime tu na wao kama wanaona ni bora wapofuke macho kwasababu wameamua kuweka hizo kope ni sawa tu, au kubaki 'natural' na kujipenda kama jinsi alivyo na kuipenda kazi yake ila siwezi kuzungumzia sana hili maana limekaa kibinafsi". 

Hayo yamejiri kufuatia kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kupiga marufuku wabunge wanawake kuingia Bungeni wakiwa na kope bandia pamoja na kucha, baada ya Mbunge wa viti maalum (CCM), Fatma Tawfik aliyeitaka serikali kutoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya vitu hivyo ambapo Spika aliwataka wabunge kuwa mfano.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad