Mudy Majuto ambaye ni mtoto wa marehemu mzee Majuto amezungumza kuhusu kikao kitakachofanyika baada ya arobaini kuhusu mirathi ya marehemu ambapo akataja shughuli nyingine ambayo mzee Majuto alikuwa akiifanya ambayo ni pamoja na kutibu watu kwa madawa ya asili yani Uganga wa kienyeji.
"Baada ya taratibu za msiba kuisha tutaitwa watoto wake wote kutakuwa na kikao na watafanya mambo ya mila atachinjwa kuku ataachwa atakaye mrukia ndio huyo atakayetakiwa kurithi mikoba ya uganga ya baba tunafanya hivyo kwasababu kabla ya kufa ajamchagua mtoto wa kurithi hiyo mikoba" mudy Majuto.
Aliendelea kusema kuwa tiba zake alikuwa anazifanyia shamba kwani alikuwa mganga vizuri lakini alikuwa afanyi sana kutokana kujikita sana kwenye mambo yake ya sanaa sema tangu alipoenda kuhiji hakufanya tena.