Kwa Mara ya Kwanza Taifa Stars Wameitwa Wachezaji 9 Wanaocheza Soka la Kulipwa


Kwa mara ya kwanza katika historia timu ya taifa imeitwa ikiwa na wachezaji tisa (9) wanaocheza soka nje ya nchi kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019.

Kutokana na ongezeko kubwa la wachezaji wa Tanzania kwenda kucheza nje ya nchi siku za hivi karibuni, nahodha wa Taifa Stars @samagoal77 amesema, tunapoelekea ni pazuri.

"Tunapoelekea ni pazuri, siku zote nilikuwa nikiomba na kupigana ili wachezaji wengi watoke Tanzania waende kucheza professional haijalishi ni wapi."

"Unapocheza kwenye ligi ambazo zimeendelea zaidi ya Tanzania kuna kitu kingine tofauti unajifunza. Unapokua kwenye ligi ya nyumbani unaweza kubadilishiwa makocha wanakuja kutoka sehemu tofauti lakini vitu ambavyo unaenda kukutana navyo kwenye ligi vinakua havina tofauti kubwa."

"Ombi langu na mawazo yangu siku zote ni wachezaji kwenda kucheza nje ya Tanzania kitu ambacho sasa hivi kinatokea, nadhani tunapiga hatua nzuri." - #regrann
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad