MWANANCHI mmoja ambaye amejitokeza kwenye mnada wa kununua makontena yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika makontena yote 20 hakubahatika kuona masofa ndani yake badala ya viti na samani nyingine.
“Tulipata fursa ya kukagua makontena yote 20 siku chache kabla ya mnada, mimi niseme ukweli tu sikuona masofa kwenye hayo makontena, lakini kuna viti ya cabinet,” alisema mnunuzi huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ibrahim.
Pia amesema bei iliyowekwa na TRA wao kama wanunuzi hawaijui, huku akidai kwamba ujazo wa makontena hayo ni mdogo. (Yana mzigo kidogo ikilinganishwa na ukubwa wake) na kuongeza kuwa iwapo ikipangwa vizuri yanaweza kutoka makontena matano au sita pekee badala ya 20 yanayotajwa.
Mnada wa makontena 20 ya Makonda umefanyika bila mafanikio, baada ya wateja kushindwa kufika bei ikiwa ni mara ya pili kwa makontena hayo kukosa wateja tangu yalipoanza kuuzwa Agosti 25.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ghala la Dar es Salaam Inland Container Depot (DIC) leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono (Auction Mart), Scholastica Kevela amesema wataendelea na mnada hadi makontena hayo yauzike.
Hata hivyo, Kevela alikataa kutaja bei ya mwisho akisema hiyo ni kazi ya Kamishna mkuu wa Mamlaka ya mapato (TRA). Mbali na makontena hayo, Kevela alisema wameuza bidhaa mbalimbali katika mnada huo na wataendelea nao wiki ijayo.
Laana ya Makonda Yaanza Kufanya Kazi.... Mnunuzi Atoboa Siri Nzito
0
September 01, 2018
Tags