Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajia kuendelea kesho Ijumaa Septemba 14 2018 kwenye Viwanja viwili.
Kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga Azam FC watakuwa wageni wa Mwadui FC mchezo utakaochezwa saa 8 mchana.
African Lyon wao watakuwa Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam kuwakaribisha Coastal Union kutoka Tanga mchezo utakaochezwa saa 10 jioni.