Lipumba akinukisha Liwale, amrushia madongo mgombea CCM na Serikali


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi CUF anayetambulika na Msajili wa vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amemtupia madongo mgombea Ubunge wa Chama cha Mapinduzi jimbo la Liwale, Zubeir Kuchauka kwa kumuita msaliti. 

Kuchauka anagombea kwa mara ya pili ubunge kwenye jimbo hilo kwa tiketi ya CCM baada ya kujivua uanachama na nafasi zake zote ndani ya CUF ikiwemo Ubunge na kujiunga na CCM kwa madai ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi. 

" Kuchauka ni msaliti, hatakiwi ndani ya CCM wala CUF na hata wananchi wa Liwale hawamtaki, njaa ya tumboni imemuendea kichwani na hivyo hafai kuwa kiongozi wenu, Mbunge wenu ni Mohamed Mtesa kutoka Chama cha Wananchi ambaye anajua shida zenu. 

" Ndugu zangu wa Liwale leo mnapata fursa ya kuwapelekea salamu CCM, ya kuwapelekea salamu Serikali, tumechoka, tumechoka kunyimwa haki zetu. Hali ya maisha ni ngumu tunahitaji mabadiliko, Liwale mtabadilisha siasa za Nchi hii kwenye uchaguzi wa Oktoba 13 kwa kumuangusha Kuchauka," amesema Profesa Lipumba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad