Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amelalamikia kufanyika hujuma dhidi ya wagombea wake waliojitokeza kuwania nafasi za Udiwani katika baadhi ya kata ambazo zina uchaguzi wa marudio.
Akifungua mkutano wa baraza kuu la chama hicho Profesa Lipumba amesema wagombea wa chama hicho katika kata ya Luwaruke, Kisiju, pamoja na kata ya njia nne wilaya ya Mkuranga wameshindwa kurudisha fomu za udiwani kwa viongozi wa kata.
"Kulivyotangazwa Uchaguzi tukasema tutaweka wagombea lakini wengine jana wakati wanarejesha fomu walikamatwa kwa madai ya kughushi muhuli, na nikitoka hapa mimi na wagombea tutaelekea tume kufikisha madai yetu, ili wasiseme mambo haya yameishia kwenye vyombo vya habari,tukihitaji demokrasia lazima tufate taratibu" amesema Profesa Lipumba.
Aidha kiongozi huyo pia amekikosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa upinzani kutangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuunga mkono juhudi za chama hicho na kusema hawana sababu za msingi.
"Eti wanajiunga na CCM kwa sababu inatekeleza mambo mazuri kwa watanzania, wakati ripoti za mwaka 2017 zinaonyesha watanzania wengi hawana furaha, mbona watanzania wenyewe wanakaribia kujinyonga kwa hali ngumu hata wafanyabiashara wenyewe wanalalamika. Mzunguko wa fedha haupo