Magufili Ambadilikia Mbunge John Heche "Toa Mkono Mfukoni"


RAIS Dkt. John Magufuli amemmtaka mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche kuwa na nidhamu wakati akizungumza na mkuu huyo wa nchi kwani ukiachilia mbali madaraka yake kwa Taifa lakini pia kiumri ni sawa na mzazi wa mbunge huyo.

 

Magufuli ametoa kauli hiyo leo Nyamongo, Tarime wakati alipomuuliza mbunge huyo iwapo wameshapeleka pesa zozote za jimbo kwa ajili ya maendeleo  ya kuchangia fedha kwa ajili ya kutatua kero katika Shule ya Sekondari Ingwe, wilayani humo mara baada ya kupokea kero kutoka mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule hiyo, Monica Bernad.


Akimjibu Rais Magufuli, Heche alisema jimbo lake tayari limeshapeleka mabati 200 na mifuko 160 ya saruji.

 

Rais Magufuli akamwambia heche;

“Toa basi mkono wako mfukoni, unajua wakati mwingine unapozungumza, wewe ni mwanangu wa kukuzaa,” alisema Magufuli kisha akapitisha harambee kwa mawaziri, wabunge, madiwani, wakurugenzi, makatibu wakuu na viongozi wa vyombo vya usalama waliokuwepo kwenye mkutano huo ambapo zilipatikana jumla ya Tsh. Milioni 29 ambazo amezielekeza zikatatue kero katika shule hiyo ya Ingwe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad