Magufuli ‘Awananga’ Waliokataa Bajeti ya Serikali

Magufuli ‘awananga’ waliokataa bajeti ya Serikali
Rais John Magufuli ametumia hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi na ukarabati wa meli kuwapongeza wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kupitisha bajeti ya Serikali huku akiwananga wabunge kutoka vyama vya upinzani kwa kupiga kura ya hapana.


Akihutubia wananchi jijini Mwanza leo Septemba 3, 2018 Rais Magufuli amesema iwapo wabunge wa CCM nao wangepiga kura za hapana kama wenzao wa upinzani, Serikali isingeweza kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa meli mpya, reli ya kisasa na ununuzi wa ndege.

"Ni demokrasia kusema hapana; lakini hiyo ni demokrasia mfu iwapo inakwamisha maendeleo ya wananchi," amesema na kuongeza, “wangepitisha bajeti na kufuatilia matumizi na utekelezaji."

Amesema kura ya hapana inamaanisha wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa waendelee kuteseka kwa kukosa usafiri wa uhakika ndani ya Ziwa Victoria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad