Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika kusini imehalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha.
Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.
Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi wamesheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''.
ini, Raymond Zondo, amesema sheria inayopiga marufuku watu wazima kutumia bangi ilikuwa kinyume cha katiba.
Serikali ya Afrika kusini bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na na uamuzi huo.
Watumiaji watatu wa bangi walikuwa wanakabiliwa na mashtaka walijitetea mbele ya mahakama hiyo wakisema '' mashataka dhidi yao yaliingilia uhuru wao''
Naibu jaji mkuu Raymond Zondo alisema: "Sio hatia kwa mtu mzima kutumia au kugusa bangi akiwa katika eneo la faraghani hasa ikiwa anafanya hivyo kwa maatumizi yake ya kibinafsi''
Licha ya uamuzi huo, ni hatia kwa mtu kuvuta au kuuza bangi hadharani.
Mahakama ya Kimataifa Afrika Kusini Yaalalisha Uvutaji wa Bangi
0
September 19, 2018
Tags