Makonda aona wivu Magufuli kwenda mikoani

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli kufanya ziara ya mara kwa mara kwa Mkoa wa Dar es salaam ili kuwawezesha wananchi wa mkoa huo kumuona kiongozi huyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matumizi ya barabara ya juu Flyover Tazara jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amemuomba Rais Magufuli kuiongeza Dar es salaam kwenye ziara zake ili aweze kukutana na wananchi wa jiji hilo.

“Mheshimiwa Rais sina mengi ya kuomba kwako zaidi ya kukuomba unapofanya ziara zako mkoani uwe unakuja na Dar es salaam walau uwe unakutana na wananchi wa Mbagala, Yombo, pamoja na maeneo mengine maana hawa huwa wanakukumbuka sana, pia huwa tunaona wivu unapofanya ziara mikoani lakini kwetu hatukuoni.”

Aidha mkuu wa huyo mkoa ameeleza Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni linaingiza shilingi milioni 800 kwa mwezi kupitia tozo zinazotolewa na watumiaji wa daraja hilo pamoja na kueleza changomoto ya utapeliunaofanywa na baadhi ya madalali Dar es salaam kwa kushirikiana na taasisi za kifedha.

Barabara hiyo ya Flyover iliyozinduliwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 90 za kitanzania na unatarajiwa kudumu zaidi ya miaka 100 na ukiwa na lengo la kupunguza adha ya foleni kwa watumiaji wa barabara ya Mandela pamoja na barabara ya Nyerere.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad