Makamu wa Rais Samia Suluhu atakuwa mgeni rasmi katika uzunduzi wa tamasha la urithi litakalofanyika kati ya Septemba 15 hadi 22 mwaka huu jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 13 2018, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge amesema kuwa Samia atamwakilisha Rais John Magufuli ambaye ndiye awali alikuwa awe mgeni rasmi.
Amesema maonyesho lengo la tamasha hilo ni kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini hususani kwa kuendeleza mazao ya utalii, utamaduni na malikale.
“Kauli mbiu ya maonyesho haya ni ‘Urithi wetu Fahari yetu’ na yatahusisha wadau kuonyesha mambo ya burudani, maigizo, utalii na tamaduni, malikale na kazi mbalimbali za mikoa,”amesema.
Amesema kutakuwa na maandamano yenye shamrashamra za ngoma, machifu, watalii, washahiri, maigizo, wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi akiwemo Mrisho Mpoto na Wanne Star.
Mama Samia umwakilisha Rais Magufuli tamasha la urithi Dodoma
0
September 13, 2018
Tags