Man Fongo Achukizwa na Sungusungu

Man Fongo achukizwa na Sungusungu
Msanii wa miondoko ya singeli, Man Fongo amesema anachukizwa tabia ya baadhi ya Sungusungu waliopo eneo Ali Maua Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa madai wamekuwa wakibambikizia wananchi kesi zisizokuwa za kweli.

Man Fongo ameeleza hayo alipokuwa anazungumza na eNewz baada ya kupita siku chache, tokea baba yake mzazi kudai kijana wake huyo amekamatwa na kuwekwa kolokoloni kutokana na kukutwa na bangi.

"Sungusungu wa Ali Maua wanafanya kazi kinyume na taratibu na wamekuwa na tabia ya kuwabambikizi wananchi kesi, naomba waondolewa tubaki na kituo cha polisi peke yake na kama kuna tatizo lolote tutaenda kushitaki polisi. Wale Sungusungu wanasumbua vijana pamoja na kina mama na walishalalamikia lakini malalamiko yao hayajasikika bado.", amesema Man Fongo.

Mbali na hilo, Man Fongo amedai kuwa Sungusungu wengi wa mjini wamekuwa wakizunguka mitaani na pindi wanapokutana na raia wanaomba pesa na endapo ukiwa huna basi wanamkamata raia huyo na kumpeleka polisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad