Manara Akerwa na TFF Kutumia Neno Hujuma Kifungo cha Meneja wa Simba ‘Hujuma Adhabu Yake ni Kifo’

Manara Akerwa na TFF Kutumia Neno Hujuma Kifungo cha Meneja wa Simba ‘Hujuma Adhabu Yake ni Kifo’
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya klabu ya Simba, Haji Manara ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF kutumia neno hujuma katika kumpatia adhabu ya kumfungia mwaka mmoja kutojihusisha na mpira meneja wa timu hiyo, Richard Robert.



Kupitia mahojiano na EFM radio, Manara amesema kuwa lugha ya hujuma iliyotumiwa na TFF siyo nzuri na wanapaswa kuangalia maneno ya kutumia.

”Tunangojea kupokea barua alafu tutalitolea tamko kwa sababu Simba hatuwezi kulikalia kimya hili jambo tutasema ama kukata rufaa ama tutasema lakini kwanza tunasubiri barua,” amesema Haji Manara

Manara ameongeza ”Unajua neno hujuma sijui maana yake, hujuma ni jambo kubwa sana, hujuma ni dhambi kuu sijui, hujuma adhabu yake ni kifo, jeshini kule ukiujumu adhabu yake ni kupigwa risasi sasa hii kwa kutumia neno hujuma peke yake hiyo imetustua watu wote Simba nadhani TFF wataangalia namna sahihi ya kutumia lugha.”

”Lugha za hujuma hazikutufurahisha sana lakini yote kwa yote wacha leo nione barua ikija tutazungumza.”

Wakati kupitia katika ukurasa wake wa kijamii wa instagram, Manara ameendelea kuonyesha kutofurahishwa na matumizi ya neno hujuma kwa kuandika kuwa bado ana maswali mengi kichwani juu ya matumizi ya neno hilo hujuma.

Kosa la kuihujumu timu ya Taifa lamuweka hatiani meneja wa Simba, TFF yamshushia rungu zito

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad