Marekani Yaliwekea Vikwazo Jeshi la China kwa Kununua Ndege na Makombora ya Urusi

Marekani yaliwekea vikwazo jeshi la China kwa kununua ndege na makombora ya Urusi
Marekani imeliwekea vikwazo jeshi la China kufuatia hatua zake za kununua ndege za jeshi kutoka Urusi pamoja na makombora ya kurushwa kutoka ardhini.

Inasema ununuzi kama huo unakiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi kujibu, tabia za Urusi nchini Ukraine na madai ya kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

Majuzi China ilinunua ndege 10 za Sukhoi Su-35 na makombora ya S-400.

China haijajiunga kwenye vikwazo ilivyowekewa Urusi kutoka Marekani na washirika wake tangu mwaka 2014.
Uhusiano kati ya Marekani na Urusi ulidorora kwa haraka baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.

Madai ya Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na kuhusika kwake kijeshi nchini Sryria kuliongeza zaidi misukosuko.


EDD na Bw Li wamejumuishwa kwenye orodha ya watu wanaowekewa vikwazo ikimaanisha kuwa mali yote wako nayo nchini Marekani yanatwaliwa na kwamba raia wa Marekani wanazuiwa kufanya biashara nao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad