Mashabiki Waombwa Kumsaidia Hawa wa Nitarejea

Mashabiki Waombwa Kumsaidia Hawa wa Nitarejea
Kama mwaka sasa umepita tangu mwanadada hawa alipowahi kutolewa katika vyombo vya habari kuwa alikuwa amekuwa kama teja kutokana na matumizi ya pombe za kienyeji zilizompelekea pia kuacha muziki na kujikuta akibaki nyumbani tu,

Baada ya hapo walimsaidia dada huyo na kwenda sober ambapo alipatiwa matibabu na kuanza kurudi katika hali yake ya kawaida lakini bado alikuwa akihitaji msaada wa hapa na pale ili kurudi kimuziki.

Sasa mapya ayameibuka kuhusu hali ya mwanadada huyu huku akionekana kuendelea kudhoofka kabisa  na hii yote ni kutokana na ukweli kuwa mwanadada huyo kwa sasa ni mgonjwa sana na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ini unaoendelea kutafuna sana afya yake.

Soudy Brown wa kipindi cha shilawadu kutoa Clouds Media amethibitisha ilo baada ya kwenda  kumtembea mwanadada huyo huku akionekana kudhoofika sana na hali yake aliyonayo kwa sasa.

Mwanadada huyo anaomba msaada kwa watu mbalimbali kwa chochcote kwa sababu ya matibabu na pia hata familia yao pia haina uwezo kwa kutoa huduma ya kila kitu.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole sana mdogo wangu, dunia hadaa ulimwengu shujaa, wote hakuna anayeijua kesho, ni wakati Platnum kujitoa na kumsaidia binti huyu badala ya kuwasaidia watu mbali, katokanae mbali na asione aibu kumsaidia huyu binti kwa sasa kakwama. Diamond upo? huyu binti utake na usitake lazima umsaidie na mungu atakaupa zaidi dunia hii wote tunapita hakuna haja ya kujiona umefaulu mtihani hapa duniani wote ni divisheni ziro kwani hakuna anayeijua kesho, kama yupo ajitokeze.Platinum utu wako unahitajika hivi sasa badala ya kulumbana na akina mabeto, huyu binti ndiye aliyefungulia njia wote hao unajidai nao lazima umuheshimu sana angekuwa mgojwa wa ukimwi nawe usingekuwepo hivi sasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad