Maskini Leodegar Tenga Ashindwa Uchaguzi CAF

Rais wa zamani wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, Leodegar Chilla Tenga ameshindwa katika uchaguzi wa kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati ya FIFA kutoka Afrika ulioendeshwa na shirikisho la soka barani Afrika, CAF.

Uchaguzi huo uliofanyika nchini Misri, umeshuhudiwa Rais wa shirikisho la soka nchini Malawi, Walter Nyamilandu akiibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa jumla ya kura 23 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Danny Jordan ambaye ni Rais wa shirikisho la soka nchini Afrika ya kusini aliyepata kura 17 katika awamu ya kwanza.

Leodeger Chilla Tenga ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) ameambulia kura 14 katika uchaguzi huo uliofanyika hii leo.

Kanuni ya FIFA inaeleza kuwa ili kiongozi awe mshindi wa nafasi hiyo ni lazima afikishe kura zaidi ya 50, jambo lililopelekea washindani wa karibu, Walter Nyamilandu na Danny Jordan kuingia kwenye duru ya pili ndipo, Walter Nyamilandu aliposhinda kwa kura 35 dhidi ya 18 za Jordan.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo, mshindi wa nafasi hiyo, Walter Nyamilandu amesema,

"Napenda niwashukuru wajumbe walionipigia kura, inaonyesha ni namna gani walivyoniamini na ninawaahidi nitaliwakilisha vyema bara la Afrika".

Siku chache kabla ya uchaguzi huo, Rais wa shirikisho la soka la nchini Ceychelles, Elvis Chetty na Nicky Mwenda wa Kenya walijiondoa katika listi ya wagombea wa uchaguzi huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad