Maskini..Mbunge Ukerewe apoteza ndugu watatu Mv Nyerere


Wakati zoezi la uopoaji miili ya wahanga wa ajali ya maji iliyotokana na kivuko cha Mv Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Kisiwa cha Ukara na Bugorora wilayani Ukerewe, Mbunge wa Ukerewe Joseph Mkundi, amesema kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati.


 Akiongea na www.eatv.tv  ameweka wazi kuwa Kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati miezi miwili iliyopita, hivyo kilikuwa sawa na kilikuwa mbioni kubadilishiwa ratiba ikiwemo kuongeza idadi ya safari ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa eneo hilo.

''Kuhusu hoja yangu niliyoitoa bungeni, ilifanyiwa kazi ambapo tulikuwa tunahitaji injini mbili ambazo zilipatikana na zikafungwa labda tu suala ambalo lilikuwa bado tunalifanyia kazi ni kuona namna gani tunaweza kubadilisha idadi ya safari'', amesema.

Aidha Mbunge huyo amesema yeye mwenyewe ni miongoni wa watu waliopoteza ndugu katika ajali hiyo ambapo amedai takribani ndugu zake watatu wamefariki kwenye ajali hiyo.

Pia ametumia fursa hiyo kutoa ushauri kuwa katika eneo la kisiwa kama hicho kuna uhitaji wa jeshi la wanamaji ambalo linaweza kuchukua hatua za haraka pale inapotokea ajali.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mhandisi Isack Kamwelwe, amesema wanategemea ifikapo saa 12:00 jioni watatoa taarifa rasmi kuhusu zoezi la uopoaji wa miili kwenye ajali ya hiyo ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozama jana huko Ukerewe.

Zaidi msikilize hapo chini akieleza zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad