Maskini...Tanzania yaporomoka kwa Nafasi 7


NA ELBOGAST MYALUKO
Timu ya taifa ya soka ya wanawake (Twiga Stars) imeshuka kwa nafasi 7, kwenye viwango vya soka  la wanawake, vilivyotolewa leo Septemba 28, 2018 na shirikisho la soka la kimataifa FIFA.


Katika viwango hivyo ambavyo hutolewa kila baada ya miezi mitatu, Twiga Stars imetoka nafasi ya 118 iliyokuwa inaishikilia kutoka mwezi Juni hadi nafasi ya 25 kwa mwezi Septemba.

Katika viwango hivyo timu ya taifa ya wanawake ya Marekani imebaki kileleni mwa viwango hivyo kwa mara ya tatu mfululizo ikufuatiwa na Brazil ambayo nayo imeendelea kubaki kwenye nafasi ya 2 kwa mara ya pili mfululizo.

Twiga Stars imekuwa haifanyi vizuri kwenye michuano ya kimataifa inayotambulika na FIFA licha ya hivi karibuni kuibuka mabingwa wa Michezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad