Mastaa na Watu Maarufu Walivyoguswa na Msiba Mzito Uliotokana na Ajali ya Mv Nyerere

Mastaa na Watu Maarufu Walivyoguswa na Msiba Mzito Uliotokana na Ajali ya Mv Nyerere
Hawa ni baadhi ya mastaa na watu maarufu walioguswa na ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea September 20, 2018 nakusababisha vifo vya watu 40 kwa mujibu wa RC Mwanza, Mongella

Mo Dewji ameandika “Inna lillahi wa inna ilaihi raji’un 🙏🏽 Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, na awasimamie abiria wote na wanaohusika kwenye shughuli za uokoaji. Tuwaombee ndugu zetu.”




Alikiba Ameandika "Nimajonzi mazito ya kuzama kwa Kivuko cha MV. Nyerere kilichokuwa kikitokea Ukerewe kuelekea Bugorola, na kusababisha vifo.
Natoa pole kwa familia pamoja na wote waliopoteza ndugu na jamaa katika ajali hiyo. Nawaombea Allah awape uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu, wakati mamlaka zinazohusika zikiendelea na jitihada za uokoaji wa wahanga wengine. MUNGU azilaze ROHO za marehemu Mahali Pema AMIN



Wema Sepetu ameandika "Inna lillahi wa inna ilaihi raji'un 🙏🏽 Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, na awasimamie abiria wote na wanaohusika kwenye shughuli za uokoaji. Tuwaombee ndugu zetu. #MvNyerere


Idris Sultan nae aliandika “Nieleweke vyovyote mtakavyoamua ila Mv Nyerere imezama kwa mipango ya Mungu ila wengi wamefariki kwa mipango yetu.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad