Baada ya presha ya game ya watani wa jadi ya Simba na Yanga kutawala kwa zaidi ya wiki moja na nusu sasa, Jumapili ya September 30 2018 ndio siku ambayo ubishi ulimalizika kwa timu hizo kukutana uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo mashabiki wa timu zote wakiwa wamejitokeza kwa wingi.
Game ya leo Simba walifanikiwa kuutawala mchezo na kupata nafasi nyingi zaidi ya Yanga, kitu ambacho kilizidisha furaha kwa mashabikiwa Simba wakiamini timu yao itaondoka na point zote tatu lakini licha ya kupata nafasi zaidi ya sita, Yanga walifanikiwa kuidhibiti Simba na kuufanya mchezo umalizike kwa sare tasa 0-0.
Hii ndio mara ya kwanza kwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera na kocha wa Simba Patrick Aussems kuziongoza timu hizo katika mchezo wa watani wa jadi (Kariakoo Derby), sare hiyo sasa inaifanya Yanga kutimiza jumla ya point 13 katika msimamo wa Ligi wakati Simba wanafikisha jumla ya point 11.
Kwa upande wa takwimu za mchezo huo Simba walipiga mashuti 10 yaliolenga lango wakati Yanga matatu, Simba walipiga jumla ya kona 11 Yanga wao wakiishia kona moja pekee, Yanga wamecheza madhambi mara 27 Simba mara 12 mwisho Simba waliufanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 62 kwa 38 dhidi ya Yanga kwa dakika zote 90.