Maua Sama na Meneja wake pamoja na Soudy Brown waachiwa kwa dhamana


Soudy Brown, Maua Sama na Meneja wake(Fadhili Kondo) waachiwa kwa dhamana ya Polisi usiku huu

Watakiwa kuripoti Kituo cha Kati (Central Police) cha jijini Dar walipokuwa wanashikiliwa kesho saa 4

Inadaiwa Polisi walimshikilia mtangazaji Soudy Brown na mwanamuziki Maua Sama kwa kosa la kusambaza video iliyonesha watu wakifanya uharibifu wa fedha za Tanzania

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar, Mambosasa alithibitisha

Ikumbukwe kuwa jana Soudy alipelekwa Mahakamani Kisutu na kufunguliwa kesi moja akituhumiwa kuendesha chaneli ya YouTube ya Shilawadu ambayo haijasajiliwa

Katika kesi ya jana ya Soudy alipewa dhamana lakini alikamatwa tena kwa kesi inayodaiwa kusambaza video hiyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad