Mwanamuziki Maua Sama Jumatatu hii hajapandishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa na wadau wengi huku wenzake Soudy Brown akipandishwa mahakamini na kusomewa shtaka moja la kutumia mitandao ya kijamii bila kuwa na kibali.
Wawili hao kwa pamoja walikamatwa na jeshi la polisi wiki iliyopita kwa tuhuma za kuidhalilisha nembo ya Taifa baada ya kupost video moja mtandaoni inayowaonyesha watu wakichezea hela za Tanzania.
SoudyBrown amesomewa shtaka moja la kuweka maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali lakini dhamana ya kosa hilo iko wazi lakini anadaiwa bado anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuwa ana kesi nyingine ya kujibu.
Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo Augustine Rwizile ameghailisha kesi hiyo hadi 18 October 2018.
Naye Maua Sama hakuletwa mahakamani leo kama watu walivyotarajia huku wadau wa mambo wakidai kesi yake nitaanza kusikilizwa katikati ya wiki hii.
Mmmoja kati ya mawakili ambao walijitokeza mahakamani hapo walidai wamewasiliana na jeshi la polisi na huwenda mrembo huyo akafikishwa mahakamani katikati ya wiki hii.
Shaffih Dauda, MX, MC Luvanda pamoja na wengine wameachiwa kwa dhamana baada ya kusomewa mashtaka ya kutumia blogs na YouTube bila kuwa na kibali.