Mwanadada huyo ambaye pia anajishughulisha na mitindo nchini humo, amepokea kile ambacho kinaongelewa kwenye mitandao kuhusu picha alizopiga zikimuonyesha akiwa amevaa mavazi ya masista (Watawa) huku akiwa ameshika sigara mkononi.
Mashabiki mbalimbali wamemvaa kwa maneno na kusema kuwa sio maadili na wala hatoi ujumbe mzuri kwa jamaii na hajaitendea haki dini ya Kikristo pamoja na masista wa dini hiyo, kwa kufanya hivyo na kuonekana kama ni udhalilishaji huku wengine wakimponda kwa kile alichokifanya.
Beverly Osu amepokea ujumbe huo kutoka kwa mashabiki na kusema kuwa “Nimezaliwa na nimekuwa nikifanya vitu vya Kikatoliki najua kuwa mnachukulia imani ipasavyo, watu inabidi wapate wasiwasi na kuombea waathirikia zaidi ya elfu moja ambao wanabakwa na kunyanyaswa na mapadri”
“Duniani kwa ujumla utakuta wahanga elfu moja wamebakwa na mapadri 300 Pennsylvania na sasa hivi watu wanaongea kuhusu picha ambayo ni sanaa, Iwapo mapadri na masista wanavuta sigara kwenye maisha ya uhalisia kitu ambacho hakijapingwa bado kama dhambi”
“Wapendwa Wanigeria sifanyi nachokifanya kwaajili ya kupata pongezi zenu, hii picha ingekuwa ya filamu ingekuwa sawa? inafurahisha pale mlipotenda dhambi kwaajili tu ya picha”