Mbatia amvimbia Makonda, agomea kuhudhuria uzinduzi mbele ya JPM


Wakati Rais Dkt. John Pombe Magufuli kesho akitarajiwa kuzindua matumizi ya barabara ya juu (Flyover) Tazara viongozi mbalimbali walipewa mualiko na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwemo Freeman Mbowe, Halima Mdee, pamoja na James Mbatia kushiriki tukio hilo. 

Mbatia alipotafutwa ili kufahamu kama angeitikia wito wa mkuu huyo wa mkoa amesema anapenda maendeleo lakini kiongozi huyo alipaswa kufuata utaratibu kutoa mwaliko kwa viongozi hao. 

“Yaani kweli mimi Mbatia nialikwe na Mkuu wa Mkoa (Makonda) kupitia vyombo vya habari sio sawa kabisa, hatukatai maendeleo lakini alipaswa kufuata taratibu kabla ya kunialika kwa kunitumia barua sio kutumia vyombo vya habari. ”, amesema Mbatia 

Mapema jana katika mkutano wake za kifedha Makonda aliwaalika baadhi ya wabunge wa Upinzani ili kuhudhuria tukio hilo ambalo linatajwa kupunguza adha ya foleni kwa watumiaji wa barabara ya Mandela na Nyerere na kusaidia kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 400. 

“ Ningependa kuona viongozi wa vyama vyote waje, akiwemo Mbatia, Mbowe, Zitto Kabwe na Halima Mdee wasisusie kama ilivyo mambo ya uchaguzi, nawaalika vyama vyote vya siasa mimi nitakuwa mwenyeji wao na tutawawekea viti ” alisema Makonda
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad