Mbatia Nae Acharuka "Ni Aibu Kusitisha Uokoaji Kisa Giza"

Ni aibu kusitisha uokoaji kisa giza - Mbatia

Ajali ya kivuko cha MV-Nyerere iliyotokea wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza na kimepelekea vifo  vya mamia watanzania waliokua wakisafiri kupitia kivuko hicho limemuibua Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi na Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia baada ya kuwa kipindi kirefu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mbunge wa huyo ameikosoa kauli ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Joel Mongela kuwa zoezi la Uokoaji lilisimamishwa kwa sababu ya giza.

“Hii ni ajali ya kujitakia, kwa sababu Mbunge wa Ukerewe alitahadharisha mapema, elimu ya Mv Bukoba, Mv-Spice ilikua elimu tosha isingepelekea kutokea ajali ya jana, haingii akilini kwa  historia ya majanga nchini, ni aibu kuona shughuli za uokoaji zinasimamishwa kwa sababu ya giza, inatia uchungu inaumiza, Tanzania ni yetu sote.”

Aidha James Mbatia amependekeza kwa serikali kuundwa kwa wakala maalum ya kushughulikia maafa Tanzania Disaster Management Agency Kama sheria ya maafa ya mwaka 2015 inavyotaka.

“Ni ajabu tumerudia makosa yaleyale ya miaka 22 iliyopita, kamati za ulinzi na usalama hawana utaalamu wa kushughulika na maafa,  tukaamua kuanzisha sheria namba 7 2015 kwa ajili ya kuunda wakala wa kushughulika na maafa ili tuondokane na mambo ya kubahatisha…”

Watu mbalimbali wameendelea kutoa salamu za rambirambi kwa watanzania waliopoteza ndugu zao kwenye ajali hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad