Mbowe 'Tumeshindwa Kupakia Jenereta Tukawasha Umeme Tukawaokoa'


Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amezungumzia kuhusu uokoaji wa wa Wananchi waliozama kwenye ajali ya MV Nyerere iliyotokea jana katika ZiwaVictoria na kuua Watanzania takribani 100.

“Tumeshindwa hata kupakia jenereta kwenye mtumbwi tukaenda kuwasha umeme tukawaokoa, au tuliridhika kwamba wote waliobakia humo ni marehemu? Huwezi kuokoa watu waliolala kwenye maji kesho yake asubuhi.
“Kwa hili la MV Nyerere, Wananchi wote tuungane tupige kelele, mtu awajibike kwa uzembe huu. Ingekuwa nchi za wenzetu, tangu jana wangekuwa wameshaadhibiwa. Chadema tunamtaka Rais achukue hatua kuwawajibisha hawa watu, ninaongea kama Mtanzania,” amesema Mbowe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad