Mbunge Ahoji Kiingereza Kutumika Mahakamani

Mbunge Ahoji Kiingereza Kutumika Mahakamani
Mbunge wa Viti Maalumu, Faida Bakari amehoji ni kwanini baadhi ya mahakama nchini zinaendesha kesi zake kwa lugha ya kiingereza wakati wa mijadala yake na kutoa hukumu.

Akiuliza swali hilo bungeni jijini Dodoma leo, mbunge huyo pia amesema Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya taifa na kinapaswa kutumika katika nyanja zote ili kukipa hadhi yake.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amesema matumizi ya lugha katika mahakama yamewekwa kwa mujibu wa sheria, Kifungu cha 13 (1) na (2) cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu Sura ya 11, lugha inayotumika kuendeshea kesi katika mahakama za mwanzo ni Kiswahili lakini pia lugha inayotumika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni Kiswahili na Kiingereza.

“Hata hivyo, shauri linaweza kuendeshwa kwa lugha yoyote kwa maelekezo ya Hakimu anayeendesha kesi katika mahakama hizo japokuwa kumbukumbu za shauri na maamuzi zinapaswa kuandikwa katika lugha ya Kiingereza.

“Aidha, kuendelea kutumika kwa Kiswahili katika mahakama zetu na hukumu kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza kunatokana na kwamba Tanzania ni Mwanachama wa Jumuiya ya Madola na inafuata mfumo wa ‘Common Law’,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad