Akiuliza swali hilo bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Septemba 6, Lyimo alisema kwa sasa wananchi wana uelewa kuhusu masuala ya ugonjwa wa Ukimwi ambapo alitaka kujua ni kwa nini serikali hairuhusu watu kujipima wenyewe kwa kipimo cha haraka (Rapid HIV Test).
“Mwenyekiti ukienda Vituo vya Afya usiku vimefungwa na kuna watu wanataka kufanya ‘chap chap’ kwa nini wasiruhusiwe wafanye vipimo hivyo ili waende kwenye shughuli hiyo wakijua wako salama,” amehoji Lyimo.
Aijibu swali hilo, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema kwa mujibu wa Sheria ya Afya, upimaji unafanyika Kituo cha Afya lakininpia serikali imeanza mchakato wa sheria hiyo ili watu waweze kujipima wenyewe.
“Lakini kumeibuka mjadala kuna wengine wanasema mtu akijipima mwenyewe ataendabkuambukiza wengine.
“Kwa hiyo kwanza tutaanza kuruhusu mtu ajipime mwenyewe lakini mbele ya Ofisa wa Afya katika Kituo cha Afya, hayo ndiyo mapendekezo tuliyotoa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tutauleta bungeni ili wabunge mtusaidie,” amesema Mwalimu.