Mbunge Goodluck Mlinga wa CCM Amtega Waziri


Mbunge wa Ulanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Goodluck Mlinga amesema kama angekuwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano angejiuzulu nafasi hiyo kama kungekuwa na shinikizo kubwa kwa wananchi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea hivi karibuni katika visiwa vya Ukara.


Mbunge wa Ulanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Goodluck Mlinga.

Mlinga ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv ambapo amesema kufuatia tukio hilo la ajali angelazimika kuwawajibisha watendaji walioko chini yake kwa kosa la kutotekeleza majukumu yao kikamilifu kabla ya kujiwajibisha mwenyewe kupitia mashinikizo ya watu.

“Kwenye kuwajibika watu wanatumia njia mbalimbali, ikiwemo kujiuzulu na kupewa barua za onyo ndio maana mtu akikosea anapewa barua ya onyo, ningekuwa waziri wa uchukuzi kabla ya kujiuzulu mimi ningewawajibisha wa chini yangu, pia ningeangalia kama napata shinikizo la kujiuzulu, ningejiuzulu tu lakini baada ya kumaliza kuwawajibisha wa chini yangu.” Amesema Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga

Aidha Mbunge huyo amewakosea baadhi ya wabunge  na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa madai kutoonekana kwenye tukio la ajali ya Mv Nyerere licha ya tukio hilo kutokea ndani ya jimbo la chama hicho kupitia Mbunge Joseph Mkundi.

“Msiba umetokea wao wanadhihaki na kuishia kutukana mtandaoni lakini hawakwenda kwenye mazishi wakati viongozi wa kitaifa walifika kule, na bahati mbaya zaidi ajali ya Mv Nyerere imetokea jimbo la Mbunge wa CHADEMA wao wapo wanakula wanakejeli tu na wengine wanakula bata nje ya nchi.” , ameongeza Mlinga.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad