Mbwana Ally Samatta Hatari Sana Atupia Matatu


Na Mwandishi Wetu, GENK
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa mabao 4-0 wa KRC Genk dhidi ya Zulte-Waregem katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena.
Samatta alifunga mabao yake katika dakika za 31, 67 na 86 wakati bao lingine la Genk limefungwa na kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 29.


Hiyo ni hat trick ya pili kihistoria kwa Samatta tangu ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Na kwa ujumla, Samatta tangu ametua Genk amekwishacheza jumla ya mechi 120 za mashindano yote na kufunga mabao 46.
Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 94 na kufunga mabao 32, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 18 mabao 12.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad