Jaji huko Pennsylvania amemhukumu jela mchekeshaji Bill Cosby kifungo cha kati ya miaka 3 na 10 kwa unyanyasaji wa kingono.
Cosby, 81, pia aliorodheshwa kuwa mtu mwenye tabia unyanyasaji wa kingono ikimaanisha kuwa ni lazima ashauiriwa katika maisha yake yote na kuwekwa kwenye daftari ya wanyanyasaji wa kingono.
Mchekeshaji huyo huyo alikataa kusema lolote hata baada ya kupeea fursa ya kufanya hivyo.
Wakati wa kusikilizwa tena kwa kesi hiyo mwezi April, Cosby alikutwa na hatia ya makosa matatu ya unyanyasaji wa kingono kwa kumlewesha na kumnyanyasa kingono Andrea Constand mwaka 2004.
Mchekeshaji huyo alitapa umaarufu miaka ya 1980 wakati alishiriki katika kipindi cha televisheni kuhusu familia ya Kimarekani yenye asili ya Afrika iliyokuwa ikiishi Brooklyn, New York.
Mwezi Juni mwaka 2017 Canstand alieleza jinsi Cosby ambaye alimuona kama mshauri wake akimpa vidonge ambavyo vilemlewesha hadi asiweze kuzuia unyanyasaji uliokuwa ukiendelea
Alisema aliacha kula, kulala na kuongea na watu. Alisumbuliwa na mawazo na kisha baadaye akaamua kumuambia mama yake kile kilifanyika.
"Bill Cosby aliichukua afya yangu na maisha yangu akayavunja,2 alema. Alinipokonya afya yangu na imani yangu kwangu binafsi na kwa wengine."
Kesi tatu ambazo Cosby alishtakiwa nazo zilijumuishea na kuwa kesi moja kufuatia makubaliano kati ya mawakili wake na waendesha mashtaka.
Mwana saikolojia Kristen Dudley alisema Cosby alionyesha dalili za matatizo ya akili na angeweza kurudia.
Kabla ya hukumu jaji aimtaja Cosby kama mtu mwenye tabia ya unyanyasaji wa kingono licha ya mawakili wake kudai kuwa umri wake Cosby na matatizo yake kuona ilimaanissa kuwa hakuwa tisho.
Hukumu hiyo ya Jumanne inamaanisha kuwa atahitaji kujiandikisha kwa polisi na kuijulisha jamii popote pale ataishi kuwa yeye ni mnyanyasaji wa kingono.
\
Mke wa Cosby Camille hakuwepo wakati wa kutolewa hukumu.
Mchekeshaji Bill Cosby Ahukumiwa Miaka 10 jela kwa Unyanyasaji wa Kingono
0
September 26, 2018
Tags