Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara Adai Muda Wowote Saed Kubenea Atajivua Ubunge wa Ubungo
0Udaku SpecialSeptember 13, 2018
Mgombea ubunge katika Jimbo la Ukonga kupitia CCM, Mwita Waitara, jana akiwa kwenye Mkutano wa Kampeni jimboni Ukonga, alidai kuwa, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea aliandikiwa Barua ya kujieleza ni kwa nini anaendelea kuwasiliana na Waitara na pia kwa nini anamhoji Mwenyekiti wa Chama? Waitara alihoji inamaana ndani ya CHADEMA hawaruhusiwi kujadili mambo ya ndani ya Chama chao?
Waitara alisikitikia tabia hiyo ya kuwakataza kujadili matumizi ya ruzuku licha ya wao wenyewe wakiwa wamechangia kupatikana kwa ruzuku hiyo.
Waitara alidai kuwa, muda wowote, Kubenea atajivua ubunge wa CHADEMA na Jimbo la Ubungo litakuwa wazi."
Waitara alieleza kuwa, ndani ya CHADEMA kuna shida, kuna udikteta na hakuna demokrasia.