Mwana habari Millard Ayo amefunguka na kusema sababu kubwa inayomfanya asiwe anamuweka mpenzi wake katika mitandao ni kutokana na mazoea aliyojiwekea mpenzi wake mwenyewe kutotaka kuwekwa katika mitandao hiyo.
Akiongea katika kipindi cha clouds 360 kutoka clouds media , Milard Ayo anasema “ninae na wala simpost kwa sababu yeye mwenyewe hapendi kuwekwa katika mitandao ya kijamii, hata yeye mwenyewe haposti sura yake popote.”
Hata hivyo akiwa kama moja ya vijana walionza jitihada za kujituma na kujikwamua akiwa na umri mdogo Milard Ayo amekuwa moja ya vijana wenye ushawishi mkubwa na kuwa mfano kwa vijana wengi sana anasema kuwa kwa sasa ndoto yake kubwa ni kufungua radio yake na ni swala ambalo kwa sasa naona hatolifanya kwa sasa kuna deni kubwa la kuifanyia mazuri clouds iliyomkuza kabla ya kanza yake.
watu wamekuwa wakiniambia nifungue radio na tv yangu lakini mimi bado ninaona kuwa nina deni kubwa sana clouds bado wananidai, mimi siidai.Clouds naona wamenifanyia mengi sana, sioni kama ninaweza kuwalipa kwaio nikifanya kazi hapa najisikiavizuri zaidi.