Mimi ni Boss Madame Hiyo Boss Lady Nawaachia Watoto Wadogo "Uwezi Kujiita Boss Lady Alafu 'Unamadanga Sponsa"

Mimi ni Boss Madame Hiyo Boss Lady Nawaachia Watoto Wadogo "Uwezi Kujiita Boss Lady Alafu 'Unamadanga  Sponsa"
Mwanadada muigizaji na mwanamitindo Jacqueline Wolpe amejigamba kuwa yeye kwa sasa ni Madam Boss na kusema kuwa wanaojiita Maboss Lady na wanadanga na masposa hao ni fake kwakuwa Bossy Lady anatakiwa kuwa na pesa zake mwenyewe anazozitafuta kwa jasho lake na kujishughurisha na sio kudhaminiwa na mtu au kupewa na mwanaume.

Wolper aliongea hayo wakati akifanyiwa mahojiano na Ayo Tv na kusema kuwa kwa hatua aliyonayo kwa sasa ana hela nyingi sasa na uwezi kumfananisha na mwanamke yeyote wa bara la Afrika.

Aliendelea kusema kuwa katika nchi hii ya Tanzania Hakuna mwanamke wa kufananishwa naye na atakayefanya hivyo atakuwa anakosea labda kama atafananishwa kuwa ni miongoni mwa wanawake mastaa wa Tanzania na sii kumuweka katika wanawake wenye hela nyingi kwakuwa kwa nchii hii hakuna mwenye lever yake kipesa.

"Sijawahi kujiita Boss Lady ila kwa sasa naweza kujiita 'AM A BOSS LADY' Siwezi kufananisha na mwanamke yoyote wa Afrika na usinifananishe na wanawake wa Kitanzania Hakuna mwanamke mwenye pesa zaidi Yangu lakini kwa kiwango nilichonfikia AM A BOSS MADAM Iyo ya Boss lady Nawaachia watoto wa dogo"

"Kikubwa ukiwa kama boss lady unatakiwa uwe na pesa yako ila ukiwa na danga sponcer alafu unajiita boss madam unafake usijitutumue unatakiwa ufanye uwe realy "

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad