Mjomba wake Davido apigwa ‘bao la mkono’ kwenye uchaguzi Nigeria


Mjomba wake na Davido, Ademola Adeleke aliyekuwa anagombea Ugavana katika jimbo korofi la Osun kupitia chama cha PDP ameshindwa kwenye uchaguzi huo na hasimu wake kutoka chama tawala cha APC, Gboyega Oyetola kuibuka mshindi. 

Davido kwa mwezi mzima yeye na binamu zake wawili B-Red na Sina Rambo ambao ni watoto wa mjomba wake huyo, wamekuwa wakimpigia kampeni mitandaoni na kutumbuiza kwenye baadhi ya kata. 

Tume ya Uchaguzi nchini humo INEC jana usiku imetangaza matokeo hayo, wakati ambao Umoja wa Ulaya ambao walikuwa kama wachunguzi wakitoa ripoti kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru. 

Tayari chama cha PDP, kimepeleka maombi Mahakamani kupinga matokeo hayo yaliyotangazwa jana na INEC, huku mataifa kama Marekani na Uingereza wakilaani vitendo vya uminywaji wa uhuru katika uchaguzi huo. 

Siku ya Uchaguzi katika jimbo la Osun zaidi ya vituo 450 kati ya 520 vya kupigia kura, wapiga kura walizuiliwa na jeshi la polisi kuingia kwenye vituo hivyo na badala yake walipewa karatasi wakapiga kura na kisha polisi kuzikusanya na kuingiza kwenye vituo. 

Hata hivyo, kuna vituo 73 Mawakala wa chama cha PDP walizuiliwa kuingia kwa sababu ya kukosa sifa ya kusimamia zoezi la uchaguzi. 

Rais wa Taifa hilo, Muhammadu Buhari tayari amempongeza, Gboyega Oyetola kwa ushindi huo kama taarifa ilivyotolewa na msemaji wake, Garba Shehu. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad