Mkuu wa Soko Jiji la Arusha Akamatwa

Mkuu wa soko Jiji la Arusha akamatwa
Mkuu wa soko kuu katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, Bw. John Ruzga, amekamatwa kufuatia agizo lililotolewa na mkurugenzi wa jiji hilo Dk. Maulid Madeni baada ya kubainika kuwahadaa wafanyabiashara katika soko hilo.

Bw. John Ruzga anadaiwa kupokea fedha za wafanyabiashara kwa kigezo cha kwenda kuwalipia ushuru na kutozifikisha halmashauri kitendo ambacho mkurugenzi ameeleza ni kinyume cha utaratibu wa serikali na mtumishi wa umma.

“Kitendo alichokifanya mkuu wa soko cha kukusanya fedha za wafanyabiashara kwa kisingizio cha kuwalipia ushuru ni kinyume na sheria na ameinyima mapato serikali hivyo naamuru awekwe chini ya ulinzi akatoe maelezo ya kina juu ya suala hili” alisema, Dk. Madeni.

Naye Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Baltazar Ngowi, amewataka wafanyabiashara katika soko hilo kudai risiti pindi wanapolipa ushuru wa vibanda.
“Kutoa pesa bila kudai risiti pia ni kosa kisheria hivyo nichukue fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara mdai risiti pindi mnapolipa ushuru wa vibanda vyenu na mnapaswa kupeleka fedha zenu wenyewe badala ya kutuma mtu ili kuepuka kadhia ya kutapeliwa ” amesisitiza Bw. Ngowi

Mkurugenzi Dk. Madeni yupo katika muendelezo wa operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato ikiwa na lengo la kuongeza mapato ya serikali na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad