Mobetto Kumburuza Diamond Mahakamani Baada Ya Tuhuma Za Uchawi

Mobetto Kumburuza Diamond Mahakamani Baada Ya Tuhuma Za Uchawi
Msanii wa Bongo movie Mrembo Hamisa Mobetto anadaiwa kuingia kwenye vita ya kisheria na Mzazi mwenzake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya sakata la uchawi.

Global Publishers wanaripoti kuwa Baada ya kutuhumiwa kuwa ni mchawi na hata clips zake zainazodaiwa kuwa ni yeye kusambazwa Kwenye mitandao ya kijamii hatimaye inadaiwa kuwa timu Mobeto inayoamini kuwa mwanadada huyo hakurekodi clip hiyo, ilikuja na hoja ya kutinga mahakamani kutafuta haki.

Chanzo kinasema ni mtu aliyesambaza clip hiyo ya sauti sambamba na wale waliyoiamini akiwemo Diamond.

Mtu anayesambaza hiyo sauti ameshajulikana, lakini na Diamond naye anatakiwa kupelekwa mahakamani maana aliwaaminisha watu kuwa hiyo ni sauti ya Mobeto.

GPL limeripoti kuwa Kwa mujibu wa wanasheria, litakalomkabili Diamond ni ‘udhalilishaji’ na kwamba licha ya kwamba hakumtaja jina Mobeto lakini mazingira yanaonesha kuwa aliyekuwa anamzungumzia katika majibu yake alikuwa ni Mobeto:

Kama unavyojua udhalilishaji siyo kosa la jinai, lipo kwenye Sheria za Mwenendo wa Makosa ya Madai au Civil Procedure Code ya mwaka 1966 iliyofanyiwa marekebisho mara kadhaa“.

Sakata hilo lilitokea wik iliyopita ambapo Familia ya Diamond ilimtuhuma Mobetto kwa uchawi na baadae kusambaza voice notes ambazo zilidaiwa kuwa za Hamisa Akichonga na mganga huku akiwa anaomba awafanyie dawa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad